FAHAMU JINSI YA KUZUIA VIPELE VYA NDEVU NA WEUSI WA KWAPA BAADA YA KUNYOA

K wa wastani binadamu anatumia miezi (5) mitano ya maisha yake kushave na ndani ya miezi hiyo mitano kwa mwanaume atashave mara elfu 20,000 katika muda wa maisha yake yote. Baadhi ya watu huchukia kabisa ikifika kipindi cha kushave kutokana na changamoto wanazozipata wakati na baada ya kushave. Kushave kuna changamoto nyingi, haijalishi ni unashave ndevu (mwanaume), sehemu za kwapa au sehemu nyeti. Changamoto hizo zinaweza kua: 1. Kupata vipele baada ya kunyoa hasa kwenye maeneo yanayozunguka kidevu, kwapani na weusi. 2. Ngozi kuwasha, kutokana na ukavu unaosababishwa na spirit au bidhaa yenye alcohol inayopakwa kweny ngozi. 3. Kupata weusi baada ya michubuko na vipele baada ya kunyoa kupona vinaacha weusi sehemu husika. Changamoto hizi zinachangiwa zaidi na bidhaa na vifaa tunavyotumia kunyolea. Sio wote wanapata vipele na weusi, ila kwa wale wenye vipele na weusi kwenye maeneo wanayoshave, hiyo inachangiwa na vitu vifuatavyo: 1.kushave bil...